Idadi kubwa
ya waandishi chipukizi nchini
Tanzania, wanakabiliwa na changamoto
moja kubwa. Nayo si nyingine isipokuwa
ni kushindwa kufikia ndoto
ya kuchapisha walau
kitabu kimoja kwa sababu
ya kutokumudu gharama
za uchapishaji wa vitabu.
Kuchapisha kitabu
chenye kiwango ( standard ) kinacho hitajika
sokoni, ambacho kinaweza kukubaliwa
na wauzaji na
wasambazaji wakubwa nchini, mwandishi
anatakiwa kwa kadirio la
chini kabisa, awe
na walau kiasi
cha shilingi LAKI
NANE hadi MILIONI
MOJA NA NUSU kutegemea na ukubwa
wa kitabu.
Kiasi hiki
kinaonekana kuwa kikubwa
mno kwa mwandishi chipukizi
ambae ndio kwanza
anataka kutumia kipaji
chake cha uandishi kujipatia fedha
kwa ajili ya
kuendesha maisha yake ya kila
siku na kupata maendeleo kwa
ujumla.
Mwisho wa
siku waandishi hawa
huamua kukata tamaa
ya kutimiza ndoto
yao hiyo adhimu
na matokeo yake
mawazo waliyo taka
kuyaandikia kitabu hufa ama kupotea.
SULUHISHO
LA CHANGAMOTO HII
Katika kukabiliana na
changamoto hii, kampuni ya
masoko ya MWALU
MARKETING & GENERAL ENTERPRISES imenzisha
program maalumu ya
kuwasaidia waandishi
chipukizi kuchapisha mawazo
yao kwenye kitabu
kwa gharama nafuu kabisa ambazo
wanaweza kuzimudu.
Badala ya
mwandishi mmoja, kutoa gharama
ya SHILINGI LAKI NANE kwa
ajili ya kuchapisha
kitabu chake, Mwalu Marketing
inawakusanya waandishi chipukizi
kuanzia kumi wenye
mawazo yanayo fanana
na kuchapisha kitabu
kimoja ambapo kila
mwandishi atatakiwa kutoa
kiasi cha SHILINGI ELFU
THEMANINI TU (Tshs . 80,000/=).
Program hii imelenga
kuwasaidia maelfu ya
waandishi chipukizi wa
vitabu nchini Tanzania, ambao wanatamani kuyaweka mawazo yao
kwenye vitabu lakini
wanashindwa kwa sababu
tu hawana uwezo wa kumudu
gharama kubwa za uchapishaji.
TUNAPOKEA MAOMBI
YA WAANDISHI CHIPUKIZI
WANAO TAKA KUSHIRIKI KATIKA PROGRAMU.
Kama wewe
ni mwandishi chipukizi ambae
unatamani kuchapisha kitabu
ama kuweka wazo
lako kwenye kitabu
lakini hauna pa kuanzia
kwa sababu ya
kutokuwa na uwezo wa
kumudu gharama kubwa za
uchapishaji, basi hii ni HABARI NJEMA SANA
KWAKO.
Kwani kupitia program hii, utaweza kuweka
wazo lako kwenye
kitabu kwa gharama
ya SHILINGI ELFU
THEMANINI TU (Tshs.80,000/=)
SIFA
ZA MAUDHUI YA KITABU
Ili kitabu chako
kiweze kukwekwa kwenye
program hii ni lazima
kiwe na sifa zifuatazo :
1.
Kiwe
na maudhui mazuri
na yenye kuvutia yasiyo kinyume
na maadili ya
mtanzania.
2.
Kiwe
na maudhui yanayo zingatia na
kufuata taratibu na sheria za
nchi.
3.
Kisiwe
na maudhui ya kisiasa
au yenye mwelekeo
wa kisiasa.
MAUDHUI YATAKAYO
PEWA KIPAUMBELE
Maudhui yatakayo pewa
kipaumbele katika program hii
ni pamoja :
1.
Riwaya
mbalimbali za kusisimua
2.
Simulizi
kuhusu historia ya
ukweli ya maisha ( IWE SIMULIZI
YENYE KUSISIMUA )
3.
Mafundisho mbalimbali
ya ujasiriamali kama vile :
i.
Utengenezaji na
utayarishaji wa bidhaa mbalimbali
ii.
Ufugaji
wa mifugo mbalimbali kama vile
kuku wa kienyeji, kuku wa nyama na kuku wa mayai, mbuzi wa nyama & maziwa, ng’ombe wa
nyama na maziwa, nakadhalika.
iii.
Kilimo
cha mazao mbalimbali ya chakula
na biashara
iv.
Fursa
za biashara mbalimbali
na ujasiriamali
v.
Uanzishaji na
uendeshaji wa biashara
mbalimbali
vi.
Uanzishaji na
uendeshaji wa makampuni
mbalimbali
vii.
Uanzishaji na
uendeshaji wa Taasisi
na mashirika mbalimbali
viii. Uanzishaji na
uendeshaji wa viwanda vidogo
vidogo vya aina
mbalimbali kama vile
viwanda vya usindikajiwa bidhaa
mbalimbali nakadhalika.
ix.
Usagaji
na upakiaji wa unga
wa mahindi, muhogo nakadhalika.
x.
Uanzishaji na uendeshaji wa
biashara ndogo za
aina mbalimbali .
xi.
Mafunzo
ya ufundi stadi.
4.
Uandishi
wa vitabu vya
kitaaluma vya masomo mbalimbali kuanzia
ngazi ya chekechea.
5.
Uandishi
kuhusu umuhimu na faida
za kusoma kozi
mbalimbali kuanzia ngazi
ya cheti nakuendelea
zinazo tolewa na
vyuo mbalimbali
6.
Uandishi
kuhusu historia na shughuli za
Taasisi mbalimbali zisizo
kuwa za kiserikali (NGOS)
7.
Uandishi
kuhusu historia na shughuli
za kampuni mbalimbali
8.
Uandishi
kuhusu utelekezaji wa
miradi ya mashirika
mbalimbali yasiyokuwa ya
kiserikali ( NGOS )
9.
Vitabu
kuhusu mafundisho ya
kidini
10.
Vitabu kuhusu mafundisho
ya afya
11.
Vitabu
kuhusu masuala ya
jadi na utamaduni
12.
Uandishi
wa mashairi ya muziki wa
bongo fleva ( Katika maudhui mbalimbali
kuanzia R& B hadi
HipHop ) :HII INAWAHUSU WATUNZI WA
MASHAIRI YA NYIMBO ZA BONGO
FLEVA AMBAO WANATAKA
KUONYESHA VIPAJI VYAO
VYA UTUNZI KUPITIA KITABU
)
13.
NAKADHALIKA.
JINSI YA KUFANYA
Fika katika
ofisi zetu zilizopo MBEZI
BEACH jijini DAR ES
SALAAM ukiwa na manuscript (
muswaada) wa kitabu chako
katika soft copy .
NA KWA MAELEZO NA
UFAFANUZI ZAIDI, WASILIANA NASI KWA
SIMU NAMBA : 0687319762
Kwa waandishi chipukizi waliopo
nje ya mkoa wa Dar
Es Salaam, ambao wanataka
kushiriki katika program hii
wasiliana nasi kwa simu yetu 0687319762 tuwape utaratibu.
WAHI NAFASI
YAKO MAPEMA,KABLA OFA
HII HAIJA FIKA TAMATI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni